VITENDO VYA UKIRITIMBA KWA BAADHI YA WATENDAJI WA SERIKALI

 

 

Makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania mhe, samia suluhu hassan ameuagiza uongozi wa mkoa wa dodoma uhakikishe unaondoa vitendo vya ukiritimba kwa baadhi ya watendaji wa serikali ambavyo vinaweza kusababisha ucheleweshaji au kukwamisha ujenzi wa miji mipya mikubwa mitano ya kisasa katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

Mhe samia akizungumza na na viongozi wa mkoa wa dodoma baada ya kupokea taarifa ya kikosi kazi kilichoundwa kwa ajili ya kuratibu shughuli za serikali kuhamia dodoma amesema ni muda muafaka  kujipanga katika kupokea wawekezaji wenye nia njema ya kuwekeza kwenye sekta mbalimbali mkoani humo.

Makamu wa rais pia ameuagiza uongozi wa mkoa wa dodoma kulinda na kuendeleza maeneo yote yenye uoto wa asili ili yasije yakaharibiwa kutokana na uwekezaji utakaofanyika mkoani humo.

Aidha ametaka kutengwe maeneo maalum kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo, ili wanufaike na mpango wa serikali kuhamia dodoma.

Mkuu wa dodoma jordan rugimbana amemweleza makamu wa rais kuwa kazi ya kuainisha maeneo mbalimbali kwa ajili ya uwekezaji, makazi na mahali ambapo ofisi za serikali na za mabalozi zitajengwa umeshakamilika