VUGUVUGU LA WANAOTAKA KUJITENGA KATIKA JIMBO TAJIRI LA CATALONIA

 

 

Waziri mkuu wa uhispania mariano rajoy ametangaza hatua anazokusudia kuzichukuwa ili kulisambaratisha vuguvugu la wanaotaka kujitenga katika jimbo tajiri la catalonia.

Rajoy amelitolea mwito bunge la uhispania  kutumia ibara ya 155 ya katiba ya uhispania ambayo haijawahi kutumiwa, inayoiruhusu serikali kuu kuingilia kwa muda usimamizi wa jimbo ikiwa viongozi wa jimbo hilo wamevunja sheria.

Ibara hiyo ya katiba, ndiyo hatua thabiti zaidi iliyochukuliwa na serikali ya mjini madrid, kuhusiana na azma ya viongozi wa catalonia kutangaza uhuru kwa msingi wa kura ya maoni iliyofanyika oktoba 1, ambayo mahakama iliitangaza kuwa batili.