KUNA UWEZEKANO MKUBWA WA KUANZISHA BENK YA VYAMA VYAUSHIRIKA

 

Serikali ya mapinduzi inakamilisha inatarajia kuanzisha benki ya vyama vya ushirika baada ya kukamilisha taratibu ili kuwanufaisha wanaushirika.

Katibu mkuu wizara ya kazi uwezeshaji wazee, vijana, wanawake na watoto fatma gharib bilali amesema kuna kiwango kikubwa cha fedha zinazowezesha kuanzishwa benki hiyo, hivyo tathmini inafanyika ili kufikia mkakati huo.

Akizungumza katika warsha ya kutathmini utekelezaji wa mpango wa kuimarisha huduma za fedha vijijini amesema ni vyema wakajifunza kutoka nchi za nje jinsi wanavyokuza miradi yao na kuweza kukuza vipato katika vyama vyao.

Mkurugenzi idara ya maendeleo ya ushirika khamis daudi amesema nivyema vyama vya ushirika wakaungana kwa pamoja na kuweza kutatua matatizo yanayowakali wanachama wake katika kujilete maendeleo.

Washiriki wamkutano huo wameelezea mafanikio waliyoyapata ikiwa ni pamoja na kuwa na kiasi kikubwa cha akiba kitakachowezesha kuendeleza mambo mbalimbali ya kimaendeleo.