VYAKULA VYA SUKARI KWA KIASI KIKUBWA UNACHANGIA KUONGEZEKA MARADHI YA KINYWA NA MENO

 

Waziri wa afya Mhe Hamad Rashid Mohamed amesema mabadiliko ya tabia na ulaji wa vyakula  vya sukari  kwa kiasi kikubwa unachangia  kuongezeka  maradhi ya kinywa na meno katika jamii.

Kauli  hiyo ameitoa katika madhimisho ya kilele cha siku ya afya kinywa na meno duniani  amesema  maradhi hayo yamekuwa yakiwathiri watu wengi na   inakisiwa kiasi cha asilimia 90 ya wananchi wote dunia wako hatarini kuugua maradhi ya meno .

Amesema wakati siku ya afya ya kinywa na meno inadhimishwa  wizara yake imekuwa na changamoto ya kukosekana kwa  madaktari katika  baadhi ya vituo vya afya vya kutibu maradhi hayo na huku hospitali nyengine zikaoneka  kutokutoa huduma kutoka na ukosefu wa vifaa.

Dakatari dhamana kanda ya Unguja   Muhidini Abdalla Mohamed amesema  maradhi ya kinywa na mdomo yamekuwa yakiongezeka kila siku hususan kwa watoto wadongo ambao mara nyingi hutumia vyakula vya sukari.

Nae dakatari mkuu wa meno kutoka shirika la hipz Dk Feroz Jaffarji amesema shirika lake litaendelea kuisaidia zanzibar  kutoa matibabu ya meno wakishirikia na timu ya madaktari ya wizara ya afya pamoja na madaktari kutoka austria.

Siku ya kinywa duniani imeenda sambamba na utoaji wa misuaki na mabuku  pamoja na kutoka huduma za meno kwa wanafunzi wa skuli mbali mbali .