VYOMBO VYA HABARI NCHINI VIMEPONGEZWA KWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI

 

Vyombo vya habari nchini vimepongezwa kutokana na kasi yao ya kuendelea kushirikiana na serikali ya mapinduzi ya zanzibar katika kuwafikishia habari za kiuchumi na kimaendeleo wananchi walioko mjini na vijijini.

Pongezi hizo zimetolewa na mkurugenzi wa mawasiliano na habari ikulu hassan khatib hassan wakati kikao cha pamoja cha kutathmini utendaji wa kazi kati ya maafisa habari wa wizara na taasisi mbali mbali za serikali waliokutana katika ukumbi wa zamani wa baraza la wawakilishi kikwajuni.

Ndugu hassan amesema mbali na vyombo hivyo kukabiliwa na majukumu makubwa ya utendaji wa kazi lakini waandishi wa habari hao wameweza kuitumikia vizuri serikali kwa kuelezea jitihada zinazochukuliwa na serikali kuwaletea maendeleo wananchi licha ya changamoto zinazowakabili.

Aidha mkurugenzi huyo wa idara ya mawasiliano na habari ikulu amevipongeza vyombo vya habari kutokana na ushiriki wao mzuri wa utoaji wa habari katika kipindi cha sherehe za miaka 54 ya mapinduzi ya zanzibar.

Mapema mkurugenzi wa idara ya habari maelezo ndugu hassan vuai amesema juhudi zaidi zinahitajika kwa waandishi wa habari kuelekeza nguvu zao katika kuandika habari zaidi za vijijini ambako wananchi wamepiga hatua kubwa kimaendeleo.

Katika michango yao maafisa hao wa habari kutoka taasisi mbalimbali za serikali wametaka kuwepo utaratibu maalumu wa kuwakutanisha maafisa wa mawasilianona habari mara kwa mara ili kutathmini mafanikio na matatizo yanayowakabili katika utendaji wa kazi zao za kila siku.