VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA VINAHITAJI KUIMARISHWA ZAIDI KIUTENDAJI

Naibu waziri afisi ya makamu wa rais anaeshuhulikia muungano na mazingira, mh luhaga jonson mpina, amesema vyombo vya ulinzi na usalama vinahitaji kuimarishwa zaidi kiutendaji kwani vimekuwa na jukumu kubwa katika kulinda usalama wa nchi.
Akizungumza na maafisa wa jeshi la polisi zanzibar, katika ziara maalum, amesema licha matatizo yanayolikabili jeshi la polisi, limekuwa likitekeleza majukumu yake kikamilifu katika kupambana na vitendo uhalifu.
Naibu kamishna wa polisi juma ali yussuf, amesema vita dhidi ya vitendo uhalifu vinahitaji ushirikiano kutoka kwa jamii kwa kutoa taarifa za haraka kwa jeshi hilo ili lichukue hatua zinazofaa.
Mh. Mpina pia amepokea taarifa za kiutendaji kutoka kwa kamishna mkuu wa idara ya uhamiaji zanzibar, johari masoud sururu, kwa kueleza kuwa wamefanikiwa kuwachukulia hatua za kisheria watu 92 wanaokiuka taratibu za uhamiaji pamoja kuimarisha utoaji wa huduma
Mh. Mpina pia ametembelea idara ya mambo ya nchi za nje na ushikiano wa afrika ya mashariki.