WAAJIRI WA MAKAMPUNI WA MAJENZI KUWALIPA VIWANGO VYA MISHAHARA WAFANYAKAZI WAO

 

 

Kamati ya maendeleo ya wanawake habari na utalii ya baraza la wawakilishi imewataka waajiri wa makampuni na wakandarasi wa majenzi kuwalipa viwango vya mishahara wafanyakazi wao kama serikali ilivyoagiza.Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua viwanda na taasisi za watu binafsi kwa ajili ya kuangalia maslahi ya wafanyakazi mwenyekiti wa kamati hiyo mh, ali suleiman shihata  amesema ni jambo la kusikitisha kuona mpaka sasa  baadhi ya waajiri wanakaidi kutekeleza agizo la serikali.

Aidha kamati hiyo imemuagiza mkandarasi wa majumba ndugu sharali shamps kuwasilisha vielelezo vya wafanyakazi ikiwemo viwango vya mishahara ndani ya wiki moja kwani amekuwa akiwatumikisha  bila ya kuwa na mikataba ya kazi.Kamati hiyo pia imetembelea kiwanda cha maji cha drop kilichopo hanyegwa mchana na kukagua  maslahi ya wafanyakazi wa kiwanda  kufuatia madai ya mwekezaji wake kutowapa stahiki  wafanyakazi kama inavyotakiwa.