WAANDAMANAJI ZIMBABWE WATAKA TUME YA UCHAGUZI IVUNJWE

Waandamanaji nchini zimbabwe wametoa wito wa kuvunjwa tume ya uchaguzi ya nchi hiyo.
Aidha wametaka kusimamishwa uchaguzi wa rais wa mwaka ujao na umoja wa mataifa na umoja wa afrika.
Waandamanaji hao wamedai kuwa tume ya uchaguzi ina mipango na serikali ya kuiba kura katika uchaguzi huo ambao rais robert mugabe anatarajiwa kugombea tena.
Mugabe amekuwa madarakani kwa miaka 30 amekabiliwa na madai ya udanganyifu katika chaguzi zilizopita.