WAANDISHI WA HABARI KUFANYA KAZI KWA UADILIFU

 

Mwenyekiti  wa  kamati ya maendeleo  ya wanawake  habari  na utalii mh ali suleiman  shihata  amewaomba  waandishi wa habari  kufanya kazi kwa uadilifu  kwa kukata vitambulisho  na kupewa leseni  ili kutambuliwa  na taasi wakati wa kupata habari kuondosha matatizo  na usumbufu kwa jamii.

mh shihata ametoa wito huo huko katika ukumbi wa wizara ya habari   alipokua akizungumza na  taasisi mbali mbali  za uandishi wa habari ikiwa ni muendelezo wa ziara  ya kukagua na kushughulikia changamoto zinazojitokeza katika tadhinia hiyo.

Amesema  kufanya hivyo kutasaidia kuondosha matatizo  yanahowakumba waandishi wa  habari kwa kupunguza  malalamiko katika utendaji kazi hiyo.

Nao washiriki kutoka taasisi za binafsi  wamesema kumekuwa na ubinafsi kutopewa ruhusa ya kushiriki kwenye  nafasi za serikalikatika utafutaji wa habari

hivyo wameomba  kamati hiyo kuangalia kwa kina ili waweze kushiriki kama vyombo vya serikali ili wapewekipaumbele zaidi