WAANDISHI WA HABARI WAMETAKIWA KUFANYA UCHAMBUZI WA KINA WANAPOANDIKA HABARI

 

Waandishi wa habari wametakiwa kufanya uchambuzi wa kina wanapoandika habari  mbali mbali zikiwemo za udhalilishaji na za watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi ili kupunguza matatizo hayo katika jamii. Akizungumza na wandishi wa habari katika mafunzo ya haki za watoto mtaalamu wa masuala ya watoto wa save the children bi neema baira amesema wandishi wa habari ni watu muhimu wa kufikisha taarifa kwa jamii hivyo amewaomba kuziandika kwa umakini zaidi kulitokomeza kabisa tatizo hilonaye  bwana dikson megera  kutota taasisi inayoshughulikia haki za watoto zanzibar amesema mafunzo hayo ya siku moja yatawasaidia waandishi wa habari kutafuta zaidi habari zinazopinga vitendo viovu wanavyofanyiwa watoto na pia kusaidia kutoa elimu kwa jamii ili wajue haki zao za msingi.