WAANDISHI WATAKIWA KUFANYA UCHUNGUZI WA KINA KUONDOA MIGOGORO

 

Waandishi wa habari wametakiwa kuwa makini katika kutekeleza majukumu yao na kuhakikisha wanaandika habari zilizofanyiwa uchunguzi wa kina ili kuondosha migogoro katika jamii.

Akizungumzia katika mkutano wa kubadilishana uzoefu katika ukumbi wa park hayati mwandishi mkongwe kutoka marekani bw kenneth cooper amesema waandishi wengi katika mataifa mbali mbali wanashindwa kuzifanyia utafiti habari zao na kuchangia kuidumaza sekta hiyo.

Aidha amewataka waandishi kutumia fursa ya teknolojia ya kisasa katika kuleta ubora wa kazi zao ili kwenda sambamba na mabadiliko ya dunia.

Afisa habari na mawasiliano ubalozi wa marekena bibi lauren ladenson amesema ubalozi wa marekeani umeamua kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari ili kuwajenga kuwa waandishi wenye uledi katika kuandika matokeo yanayojitokeza ndani na nje ya nchi.

Viongozi i wa klabu ya waandishi wa habari zanzibar wamesema mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo waandishi yatasaidia katika tasnia ya habari kwa kuandika habari za uchunguzi na za vijijini ambazo mara nyingi zinakosekana.
Mafunzo hayo ya siku moja yaliyoandaliwa na ubalozi wa marekana kwa kushirikiana na klabu ya waandishi wa habari zanzibar ni mpango maalum wa kutoa elimu kwa waandishi wa habari katika kuyafahamu majukumu yao.