WAATHIRIKA NA MAAFA YA MVUA WAPATIWA MSAADA

Wananchi walioathirika na maafa ya mvua za hivi karibuni katika maeneo mablimbali ya unguja wamepatiwa msaada wa vyakula ikiwa sehemu ya kuwafariji na athari hizo.
Msaada huo umetolewa na taasisi ya mwezi mwekundu ya nchi za falme za kiarabu uae ikiwa ni mchango wa wafanyabishara wa nchi hizo umegaiwa kwa zaiaidi ya wananchi mia nne wa wilaya kusini na kaskazini unguja B.
Wakipokea msaada huo kwa niaba ya wananchi hao mkuu wa wilaya ya kusini idrisa kitwana na wa kaskazini B issa juma ali wamesema msaada huo ni muhimu kwa wananchi hao ukizingatia hali zao zipo chini kutokana na maafa hayo.
Wamefahamisha kuwa msaada huo unathibitisha nchi za falme za kiarabu zipo karibu na zanzibar katika kusaidia maendelo ya wananchi. Msaada huo umesambazwa na taasisi ya milele foundation ambapo waratibu wake wamesema wafanyabiashara hao wako tayari kusaidia nyanja nyengine na kutoa pole kwa wananchi waliopatwa na maafa .