WABUNGE WA MAREKANI WAMEUTAKA UTAWALA WA DONALD TRUMP KUREJESHA VIKWAZO VYA KUSAFIRI

 

Wabunge wa marekani wameutaka utawala wa rais donald trump kurejesha vikwazo vya kusafiri dhidi ya viongozi wa kijeshi wa myanmar kutokana na wanavyowatendea waislamu wa rohingya

Marekani na umoja wa ulaya zinatafakari kuweka vikwazo vinavyolenga maeneo maalumu lakini wana wasiwasi wa kuathiri uchumi wa nchi hiyo na kudhoofisha mahusiano ambayo tayari ni ya wasiwasi kati ya kiongozi wa myanmar na jeshi.

Myanmar imekana madai ya safisha safisha ya kikabila na mauaji dhidi ya kundi hilo la kikabila, ambao maelfu wamelikimbia jimbo la rakhine na kukimbilia nchi jirani ya bangladesh.