WAFANAYABIASHARA WA SOKO LA DARAJANI WAMETAKIWA KUFUATA MFUMO MPYA WA KULIPIA USHURU

 

wafanayabiashara wa soko la darajani wametakiwa kufuata mfumo mpya wa kulipia ushuru na kuachana na mfumo wa kizamani wa kulipia ada hiyo kila siku.

hayo yamesemwa na mkurugenzi wa baraza la manispaa mjini nd. said juma ahmada wakati akizungumza na uongozi na wafanyabiashara wa soko hilo.

amesema baraza la manispaa mjini limeamuamua kuweka mfumo wa kulipia ushuru kila mwisho wa mwezi na kuachana na mfumo wa kulipia kila siku jambo ambalo litatoa fursa kwa wanyabiashara  kuwa na uhuru sambamba na kuzuia mianya ya uvujaji wa mapato.

amesema baraza la manispaa mjini linamajukumu la kuimarisha huduma kwa wananchi wa manispaa hiyo hivyo ni vyema kuendana na mfumo mpya wa ukusanyaji wa mapato itakayowezesha upatikanaji wa fedha za kutosha ili kufanikisha utoaji wa huduma zilizobora.

nao wafanyabiashara wa soko hilo wamesema licha ya kuwa mfumo huo ni mzuri lakini unawapa ugumu kuzikusanya pesa na kuzilipa mwisho wa mwezi kutokana na fedha wanazozipata zina matumizi mengi katika familia.

hata hivyo watatoa ushirikiano wa kutosha kwa baraza hilo ili kufanikisha malengo yaliyowekwa.