WAFANYA BIASHARA MAARUFU NCHINI WAMEJENGA TABIA YA KUKWEPA KULIPA KODI

 

Kamishna wa  bodi ya mapato zanzibar ndugu amour hamil bakar amesema   baadhi ya wafanya biashara maarufu nchini wamejenga  tabia ya kukwepa kulipa kodi kwa    visingizio mbali mbali.

Akizungumza katika mkutano na  wakurugenzi wa halmashauri  za wilaya wahasibu na manispaa huko kwa mchina  ,amesema serikali inategemea  mapato kwa ajili ya kuendeshea shughuli za maendeleo  hivyo,lazima kuwepo ushirikiano utakaowezesha mapato yanakusanywa kwa wingi.

Aidha amewataka watendaji wanaohusika na ukusanyaji wa mapato hayo kuwa waaminifu kwa kuhakikisha  mapato hayo hayapotei. Wakati.

Nao wakurungezi na wahasibu walioshiriki katika mkutano huo  wameelezea changamoto zilizopo katika ukusanyaji wa kodi  na kuutaka uongozi wa zrb kuzidi  kuwapatia elimu wananchi juu ya ulipaji kodi.

Naye  naibu katibu  mkuu ofisi ya rais tawala za mikoa  na serikali za mitaa na idara maalum smz ndungu kai mbarouk amesema  kuna umuhimu wa kujulikana wafanya biashara ili kuweka hesabu sahihi.