WAFANYA BIASHARA WA DARAJANI WASHINDWA KUKODI MILANGO YA MAENEO HAYO

 

wafanya biashara wadogo wadogo wa maeneo ya darajani wamesema   watashindwa kukodi milango ya maduka katika maeneo  ya darajani kutokana na kutokumudu bei ya kodi katika milango hiyo.

kauli hiyo imekuja kufuatia kuzinduliwa kwa  jengo  la treni la darajani  lenye milango ya maduka ambapo bei yake imepangwa kuwa shilingi laki nane kwa kila mlango.

wakizungumza na zbc wamesema bei hiyo ni kubwa na serikali inapaswa ifikirie  eneo jengine  la mjini kwa ajili ya  wafanyabiashara hao wadogo wadogo itakayokuwa na bei ya kiwango cha chini  watakacho kimudu kulipa.

hata hivyo wafanya biashara hao wamempongeza  rais wa zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi dk ali mohd shein kwa uamuzi wa kulifanyia matengenezo jengo la zamani jumba la treni huku wengine  wakiomba pia kuiangaliwe na banda la soko la kuku kwa vile nalo liko katika hali mbaya.