WAFANYA BIASHARA WANAHITAJI KUWA WABUNIFU KATIKA KUJIENDELEZA KITAALUMA

 

 

Katika kuhakikisha wafanya biashara wadogo wadogo   wanazalisha bidhaa zilizo bora na zenye kuleta tija, wanahitaji kuwa wabunifu katika kujiendeleza kitaaluma ili kufikia kiwango bora za azalishaji wa  bidhaa zinazouzika katika soko

Kauli hiyo imetolewa na mratibu wa shughuli za maendeleo katika  mradi wa kuwasaidia wajasiriamali kupata huduma kwa hati punguzo kutoka kwa watoa huduma na washauri wa kibiashara (engen) mw. Abass makame wakati akifunga mafunzo kwa wafanya biashara hao  yaliofanyika katika ukumbi wa skuli ya haile salasie.

Amesema ili kufikia malengo mazuri ya kibiashara ni vizuri kwa wafanyabiashara  kujiunga pamoja katika vikundi hatua ambayo  itaweza kuwasaidia na kuweza kubuni mbinu za miradi  ambazo zitasaidia kuengeza uzalishaji.

Katibu wa jumuiya ya changamoto nd. Hawana ramadhan na mwenyekiti nd. Bakari said wamesema ni vizuri wafanya biashara hao kuitumia elimu hiyo kwa vitendo ili kuweza kubadilika kibiashara.

Aidha viongozi hao wamesema wamebaini kuna baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakikata tamaa mapema baada kuona wanapata tatizo jambo ambalo haliwezi kuleta manufaa.

Katika mafunzo hayo wafanya biashara hao wamepewa mbinu mbali mbali za kuweza kuwasaidia katika biashara zao pindi wanapohitaji mikopo, mbinu  ambazo imetolewa  na mkufunzi  kutoka jumuiya ya changamoto nd. Said ali ussi.