WAFANYABIASHA BIASHARA WAMEIOMBA SERIKALI KUWAPUNGUZIA KODI

 

Wafanyabiasha biashara wa eneo la kiponda darajani wameiomba serikali kuwapunguzia huduma za kodi kutokana kushuka kwa hali ya biashara.

Akizungumza na kamera ya biashara na uchumi mfanya biashara wa darajani shoppng center ndg.nassor khassim salum amesema hali yao ya biashara kwa sasa haipo vizuri ukilinganisha na nyakati za sikukuu kutokana na wateja wengi kuishia maeneo ya vikokotoni hali ambayo inawafanya kukosa soko katika maduka yao.

Hata hivyo ameiomba serikali kupitia taasisi husika kuwapunguzia viwango vya ulipaji wa kodi ili wapate unafuu wa kuendesha biashara zao vizuri ukilinganisha na sasa kodi ipo juu kitendo ambacho kinawafanya kushindwa kumudu kwani wengi wao ni wananchi wa hali ya chini.