WAFANYABIASHARA KUDUMISHA USAFI KATIKA SEHEMU ZAO ZA BIASHARA.

 

 

Mkuu wa mkoa wa kaskazini pemba mhe omar khamis othman amewataka wafanyabiashara watakao bahatika kupewa milango na vikuta katika soko kuu la  matunda wete kudumisha usafi katika sehemu zao za biashara.

Amesema utaratibu wa sasa wa biashara katika soko hilo unahitaji usafi wakati wote kwani vyakula vya aina ya nafaka vitamiminwa katika vikuta vya kufanyia biashara.

Mh. Omar ametowa wito wete wakati akizungumza na wafanyabiashara wa eneo hilo katika mkutano wa kupata maelezo juu ya kulitumia soko kuu  la matunda wete kwa ajili ya kufanya biashara na kusisitiza suala la ulipaji wa kodi bila ya kulazimishwa.

Aidha mhe omar ametumia fursa hiyo kwa kuwatoa hofu wafanyabiashara hao kwamba katika utoaji wa milango na vikuta , imezingatia zaidi kuwapatia  wafanyabiashara waliokuwapo  katika soko  kongwe lililovunjwa .

Wakichangia katika mkutano huo wafanyabiashara hao mbali na kupongeza  uwamuzi wa serikali wa kuruhusu kuanza kulitumia  soko hilo pia wameliomba baraza la mji wa wete kuimarisha ulinzi ndani ya soko baada ya muda mauzo kuisha .

Soko kuu la wete limefunguliwa kwa ishra ya kukatwa utepe na kuwekwa jiwe la msingi na rais wa zanzibar na mwenyekti wa baraza la mapinduzi dr. Ali mohamed shein kwenye shamra shamra za kuadhimisha miaka 53 ya mapinduzi ya zanzibar.