WAFANYABIASHARA NCHINI MALAWI, WAMESEMA BIASHARA HUENDANA NA MSIMU

 

Wafanyabiashara wa mboga mboga katika soko la mponda gaga wilaya  ya  kotakota mkoa wa kati  nchini malawi, wamesema hali ya kibiashara katika soko hilo huendana na msimu wa mavuno licha ya kuwa na soko dogo lisilokidhi mahitaji.

Wakitoa maelezo yao wakati walipohojiwa na camera ya biashara na uchumi ya zbc, wafanya biashara hao wamesema msimu wa mavuno ya mpunga yanapokuwa mazuri hupata wateja  wengi na akuchangia kuongeza kipato chao cha maisha.

bei ya dagaa katika soko la mponda gaga  funguu ni shilingi mia mbili ambapo kwa pesa za tanzania  ni shilingi mia sita lakini pia kwa fungu  la tungule ni shilingi 100  kwa fedha ya malawi.

Chifu mponde wa baadhi ya eneo la kotakota katika  kijiji cha mpondagaga, amesema wakaazi wa wilaya ya kotakota wengi wao wamekuwa wakitegemea kilimo cha mpunga kwa ajili ya kuwaengezea kipato lakini kwa chakula ni muhogo na mahindi.

chifu huyo ameendelea kufahamisha kuwa mbali na kilimo pia wilaya ya kotakota wananchi wake wamekuwa wakijishugulisha na masuala ya uvuvi  .

Malawi ina mikoa minne ambayo ni kusini, mkoa wa kati, mkoa wa kaskazini na , mkoa wa mashariki ambao ni mkoa mpya kwa sasa hapo zamani ilikuwa na mikoa mitatu.