WAFANYABIASHARA WA SOKO LA KUKU DARAJANI WAMEANZA KUPATWA NA WASI WASI

 

Wafanyabiashara wa soko la kuku darajani wameanza kupatwa na wasi wasi  wa kukosa maeneo yao  ya  awali ya kufanyia biashara  baada ya  kupata taaarifa ya soko  hilo   kutaka kufanyiwa matengenezo.

Wamesema kutokana na uzoefu wao   wanachokihofia ni kutokuredishwa katika maeneo yao ya zamani  ya biashara  wakati  ujenzi wa  soko hilo utakapokamilika.

Wafanyabiashara  hao wameiambia zbc kuwa  ikiwa hakutokuwa  na uwezekano wa kuendelea na biashara zao wakati wa matengenezo hayo wameomba kupatiwa eneo jengine hadi  utakapo malizika ujenzi wa soko hilo.

Wamesema kutokana na ugumu wa hali zao za kimaisha   ikiwa hatorejeshwa katika soko hilo watakuwa hawana pakuelekea kuendelea na biashara zao hizo  huku wakiwa wanategemewa na familia zao.

Hata hivyo  wafanyabiashara hao wamelalamikia    kutoridhishwa na  hali ya  mazingira ya  soko hilo na kusema kuwa bado  yanahitaji kufanyiwa   usafi ili wateja na wageni waweze kuvutika na huduma zinazotolewa na wafanyabiashara hao.

Soko hilo bado halijawahi kufanyiwa matengenezo licha ya kuwa na uchakavu wa muda mrefu.