WAFANYABIASHARA WAMESEMA MZUNGUKO WA FEDHA UMESABABISHA BIASHARA KUWA NGUMU

Wafanyabiashara katika soko la mwanakwerekwe wamesema mzunguko wa fedha umesababisha hali ya biashara kuwa ngumu na kushuka kwa mauzo.
Wakizungumza na kamera ya biashara na uchumi sokoni hapo wamesema hali ya biashara katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa ramadhani imekuwa tofauti na ramadhani zilizopita kama wanavyoelezea baadhi ya wafanyabiashara hao.