WAFANYABIASHRA NA WABUNIFU WATAKIWA KUJITOKEZE KATIKA TAMASHA LA BIASHARA LINALOTARAJIWA KUFANYIKA

 

Waziri wa biashara na viwanda mh Amina Salum Ali amewataka wafanyabiashra na wabunifu wa vitu mbalimbali kujitokeze kwa wingi ktka tamasha la biashara linalotarajiwa kufanyika tarehe 1/2/2019 hapa zanzibar

Akizungumza  na waandishi wa habari katika ukumbi wa wizara wa biashara na viwanda migombani amesema serikali ya mapinduzi ya zanzibar kupitia wizara ya biashara na viwanda inatarajia kufanya tamasha hilo ikiwa na lengo la kuhamasisha wazalishaji wa ndani  kuzingatia ubora wa bidhaa zao wanazozizalisha.

Mh amina amefahamisha kuwa umuhimu mwengine wa tamasha hilo kutoa nafasi kwa wafanyabiashara kuweza kuzitangaza bidhaa zao ndani na nje ya nchi na kuweza kukutana na wanunuzi mojakwa moja kwa ajili ya kupata soko la ukakika

Katibu mkuu wa wizara hiyo juma ali juma akilitolea ufafanuzi amesema kwa sasa wizara imejipanga ipasavyo katika swala zima la kuwainua wajasiriamali katika kwa kuwajengea uwezo wa uzaklishaji.

Tamasha hilo la kumi na tano ambalo litafanyika katika viwanja vya maisara litajumuisha  wfnyabiashara mbalimbali wa ndani na nje ya nchi ambapo kauli mbiu ya tamasha hilo zingatia uzalishaji wa viwango kwa uakika wa soko