WAFANYABISHARA WA KILIMO CHA MCHICHA WANAKABILIWA NA UHABA WA MAJI

Wafanyabishara wa kilimo cha mchicha fuoni uwandani wanakabiliwa na uhaba wa maji kwa ajili ya kuendeleza kilimo hicho kinachowaingizia kipato.
Baadhi ya wakulima hao wamesema kutokana na tatizo hilo linalotokana na ukosefu wa mipira wa kusambazia maji na kisima cha maji cha kutosha wakati kilimo hicho kinahitaji maji mengi.
Wamefahamisha kuwa hali hiyo inawasababishia kushindwa kufikia lengo la uzalishaji walilojiwekea na kupata hasara kubwa kwa vile wanatumia gharama kubwa kuendeleza kilimo chao cha mchicha.
Mbunge wa jimbo la dimani mh. Juma ali juma amezungumza na wafanyabishara hao na kuwataka kuwa wavumilivu kwa vile uongozi wa jimbo hilo unaandaa mikakati ya kulitatua tatizo hilo.