WAFANYABISHARA WALIOMO KATIKA MFUMO USIO RASMI WAMEHIMIZWA KUJISAJILI

 

Wafanyabishara waliomo katika mfumo usio  rasmi wamehimizwa kujisajili katika baraza la kusimamia mfumo wa utoaji wa leseni ili kuingia katika mfumo wa biashara unaotambulika na kupata mikopo ya benki.

Katibu mtendaji wa baraza la kusimamia mfumo wa utoaji wa leseni ndugu rashid ali salim ametoa kauli hiyo kwenye mafunzo ya wajumbe wa kamati ya fedha, biashara na kilimo ya baraza la wawakilishi .

Amesema serikali imeanzisha baraza la kusimamia mfumo wa biashara kwa lengo la kuwaondoshea wafanyabiashara wakubwa na wadogo usumbufu wa kujisajili na wameweka masharti nafuu ili kila mmoja aweze kuyatekeleza.

Akifungua mafunzo hayo waziri wa biashara, viwanda na masoko balozi amina salum ali amelitaka baraza la kusimamia mfumo wa utoaji leseni kuweka mfumo uliowazi na rahisi wa elektroniki katika utoaji wa leseni.

Amesema mfumo wa zamani wa kutoa leseni ulishindwa kuwafikia wafanyabiashara wengi hasa wadogo ambao wana   mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa