WAFANYAKAZI 21 WAMEFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA BAADA YA KUDAIWA KUPOTEA KWA MALI ZA SERIKALI

Wafanyakazi 21 wamefikishwa katika vyombo vya sheria baada ya kudaiwa kupotea kwa mali za serikali na fedha za umma mwaka 2016 katika wizara ya fedha na mipando.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu utekelezaji wa ukusanyaji wa mapato na matumizi ya serikali kwa robo ya kwanza ya mwaka 2017 /2018 waziri wa wizara hiyo dk. Khalid salum muhammed amesema wizi huo wa fedha za serikali umebainika katika uchunguzi uliofanywa na vyombo vya sheria na kugunduaa upotevu wa shilingi bilioni moja nukta sita moja tisa.
Hata hivyo dk khalid amewasisitiza watendaji wa serikali kutojihusisha na vitendo vya rushwa na badala yake wafuate maadili ya kazi na taratibu za kisheria.
Akizungumzia suala la mapato na matumizi ya serikali kwa robo ya kwanza ya 2017/ 2018 amesema serikali imetumia zaidi ya bilioni moja ikiwa ni ongezeko la asilimia 38 kwa mwaka jana kwa shughuli mbalimbali za maendeleo.
Aidha dk khalid amesema sheria mpya za ununuzi na uondoshaji wa mali za serikali namba 11 ya mwaka 2016 na sheria ya fedha za umma ya mwaka 2016 zimeanza kutumika rasmi kuanzia julai mwaka huu.