WAFANYAKAZI WA KUTOA MISAADA WAMEANZA KUWAONDOA WAGONJWA WENYE MAHITAJI YA DHARURA

 

Wafanyakazi wa kutoa misaada wameanza kuwaondoa wagonjwa wenye mahitaji ya dharura katika eneo lililozingirwa la waasi nchini syria la ghouta mashariki,   baada ya miezi kadhaa ya kusubiri kuchukua hatua hiyo ambapo kiasi ya watu 16 walifariki..

Msafara wa magari ya kubebea wagonjwa umeanza  kuwaondoa wagonjwa walio katika hali mbaya.

Chama cha wauguzi wa syria na marekani na shirika la kutoa msaada wa kitabibu, yamesema uondoaji huo unahusisha wagonjwa 29 ambao wako katika hali mbaya, walioidhinishwa kuondolewa kwenda mjini damascus.

ghouta mashariki ni moja kati ya maeneo ya mwisho ambayo ni ngome kuu ya waasi nchini syria na limekuwa katika mzingiro mkali wa majeshi ya serikali tangu mwaka 2013, hali inayosababisha ukosefu mkubwa wa chakula na matibabu kwa wakaazi wapatao laki 4.

Shirika la hilali nyekundu la syria limesema shughuli hiyo ya kuwahamisha wagonjwa ni kufuatia kufanyika mazungumzo marefu.