WAFANYAKAZI WA TAASISI NA SERIKALI KUFANYA KAZI KWA KUZINGATIA SHERIA

 

Katibu mkuu  ofisi ya makamu wa pili wa raisi dr, idrissa muslim hija  amewataka   maafisa  na wafanyakazi wa  taasisi mbali mbali  za serikali  kufanya  kazi  kwa kuzingatia  sheria na kanuni  za utumishi  serikalini.

Akizungumza katika kikao cha kuwaaga wafanyakazi  wa wilaya ya kusini unguja wakiwemo madiwani na watendaji wengine katika vikao vilivyoanyika kitogani na makuduchi dr  idrissa amesema endapo seria  na kanuni zitazingatiwa  ufanisi wa kazi utapatikana.

amewahimiza watendaji hao kuendelea  kujituma kwa ari sambamba na kujiendeleza kielimu kwani elimu ni chachu ya maendeleo ya kila jambo.

Kaimu mkuu  wa mkoa  kusini unguja mhe,  idrisa  kitwana  mustafa  ameahidi kuyaendeleza  masuala ya serikali za mitaa na  mazuri  yote kwa faida ya taifa na wananchi kwa jumla