WAFANYAKAZI WA (ZBC) KITUO CHA DAR ES SALAAM KUPAMBANA NA MAZINGIRA MAGUMU

 

Waziri wa habari utalii utamaduni na michezo mh. Rashid ali juma amewataka wafanyakazi wa shirika la utangazaji zanzibar (zbc) kituo cha dar es salaam kupambana na mazingira magumu wanayokutana nayo katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Akijibu hoja na chanagamoto zinazolikumba shirika mbele ya kamati ya wanawake, habari na utalii ya baraza la wawakilishi ambayo imetembelea kituo hapo na kuzungumza na wafanyakazi, waziri rashid amesema shirika lina changamoto nyingi kwa sasa kutokana na maboresho ambayo yanafanywa lakini ni matarajio yao kuwa hali itabadilika hapo baadae .

Kwa upande wao wajumbe wa kamati walihoji juu ya changamoto za kituo hicho ikiwemo suala la kutokidhi viwango vya studio iliyopo kituoni hapo, na suala la utata wa zbc2 ambapo naibu mkurugenzi bi nasra moh`d alitoa ufafanunuzi ufuatao.

Katika kiako hicho mkuu wa kituo msangu saidi alipata fursa ya kueleza jinsi kituo cha zbc dar es salaam kinavyofanya kazi.