WAFANYAKAZI WAMETAKIWA KUJITOKEZA MARA KWA MARA KWENDA KUPIMA AFYA ZAO

 

Wafanyakazi wa tasisi mbalimmbali wametakiwa kujitokeza mara kwa mara kwenda kupima afya zao ili kupunguza mambukizi ya vvu na ukimwi na serikali  kuweka  mikakati malum kila taasisi kutenga bajeti yake  kwa kupatiwa mafunzo   wafanya kazi hao ili kuwa na uelewa kwa kujikinga na janga la ukumwi.

hayo yamelezwa  na naibu  waziri  wa nchi ofisi ya makamo wa pili wa rais mh,  mihayo  juma n,hunga  wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa kuzishirikishatasisi mbali mbali za serikali  kwa kuwapatia mafunzo wafanyakazi hao  yaliyoandaliwa na  ofisi ya makamo wa pili wa rais.

Kwa upande wake mkufunzi wa mafunzo hayo ndugu sihaba sadaati amesema kuwa zanzibar ukimwi bado upo  hivyo ipo haja ya kuzidisha jitihada ili kuhakikisha unapungua kwa kiasi kikubwa ingawa  utafiti unaonesha zanzibar ukimwi  kupungua kwa asilimia o.4  na idadi kubwa walioathirika hasa wanawake vijana kuanzia umri wa miaka kumina tano nakuendelea  mbele ,hivyo ipo haja waliopewa mafunzo kutoa elimu kwa wengine  ili kufikisha ujumbe.

nao washiriki wa mafunzo hayo  wameelezea hisia zao pamoja na kutoa ushauri wao kwa jamii jinsi ya kuchukua hatua na kujikinga kwa vizazi  vya sasa na baadae.

Akifunga semina hiyo ya siku moja   katibu  mkuu wa ofisi ya makamu wa pili wa rais  dk idrisa muslim hija    amesema ni vizuri kuitumia elimu hiyo na kuisambaza kwa jamiii ili itumike kupunguza  vvu na ukimwi na kusisitiza  kujiepusha na vitendo vya ngono vinavyo sababisha kuogezeka kwa kasi maambukizi hayo.