WAFANYAKAZI WANAPASWA KUJITAHIDI KUTEKELEZA MAJUKUMU YA UTUMISHI WA UMMA

Makamu wa pili wa rais wa zanzibar balozi seif ali iddi amesema wafanyakazi wanapaswa kujitahidi kutekeleza majukumu ya utumishi wa umma kwa kufanya kazi kizalendo na ushirikiano ili kujijengea mazingira bora ya hatma yao ya baadae.
Amesema tabia hiyo njema itawapa heshima kubwa katika jamii kiasi kwamba wamalizapo muda wao wa utumishi watajikuta wakiacha athari inayoendelea kukumbukwa kwa wema na watumishi wenzao waliowaacha.