WAFANYAKAZI WATAKIWA KUACHA KUFANYA KAZI KWA MAZOEA NA BADALA YAKE KUFUATA MPANGO KAZI WA IDARA

 

Mkurugenzi idara ya maendeleo ya uvuvi zanzibar, Mussa Abudu Jumbe, amewataka wafanyakazi wa idara hiyo pemba kuacha kufanyakazi kwa mazoea na badala yake kufuata mpango kazi wa idara .

mkurugenzi  Mussa ameyasema hayo kwenye mkutano wa maafisa wa vitengo vya idara hio, katika ukumbi wa wizara ya kilimo weni, wete pemba.

amesema serikali imetenga jumla ya shilingi milioni miambili na ishirini,kwa ajili ya kuendeleza shughuli za maendeleo ya uvuvi pamoja na kilimo cha mwani pemba ,lakini maafisa hao hawajazitumia  kuwafikishia taalumawananchi kama ilivyokusudiwa.

afisa uvuvi wilaya ya wete, vuai othman haji, na mkuu wa diko bandari ya wete, hamad khamis hassan wamesema wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo usafiri na vitambulisho.

nae mkuu wa idara ya maendeleo ya uvuvi pemba, sharif mohd faki na afisa kitengo cha mazao ya baharini hidaya hamad ali, wameahidi kuyafanyia kazi maelekezo yaliotolewa kwa lengo la kuleta ufanisi uliokusudiwa na serikali.