WAFUASI WA RAILA ODINGA LEO WAMEKUSANYIKA WAKIWA NA NIA YA KUMUAPISHA KUWA RAIS

 

 

Wafuasi wa kiongozi wa upinzani nchini kenya raila odinga leo wamekusanyika katika bustani katikati ya mji wa nairobi, wakiwa na nia ya kumuapisha kuwa rais, kiongozi wao ambaye alisusia uchaguzi wa marudio wa mwaka jana.

Rais uhuru kenyatta aliapishwa kutawala kwa muhula wa pili mwezi novemba baada ya kushinda uchaguzi wa marudio mwezi oktoba ambao raila odinga aliususia kutokana na shaka kwamba hautakuwa huru na wa haki.Licha ya kuwa polisi imepiga marufuku mkusanyiko wowote kinyume na sheria leo, lakini hakuna polisi katika bustani hiyo na wala polisi wa kuzuwia ghasia ama gari.Taarifa zinasema kuwa wafuasi hao wamepewa ruhusa na maafisa wa kenya kuutumia uwanja huo.