WAFUGAJI WAMELALAMIKIA MFUMUKO WA BEI YA CHAKULA CHA KUKU

 

 

Wafugaji wa kuku wa mkoa w a kaskazini unguja wamelalamikia mfumuko wa bei ya chakula cha kuku kwa wafanya biashara wa chakula hicho jamboambalo linarejesha nyuma ufugaji wa kuku hapa nchini.

Wakizungumza walipotembelewa na wanakikundi cha hapa kazi cha donge nyimbi wafugaji haji khamisi haji wa kendwa na miza mussa fumu wa kikobweni wamesema tatizo la mripuko wa bei unaojitokeza hivi sasa ni miongoni mwa  changamoto  kubwa inayowakabili wafugaji wa kuku hivyo wameiomba mamlaka  husika kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo.

Kwa upande wake mwanaharusi haji mohamed  wa kikundi cha hapa kazi amesema amenufaika  na ziara hiyo  kwa kuwa amejifunza mengi kuhusu ufugaji wa kuku na ataitumia elimu hiyo aliyo ipata kwa  kuboresha ufugaji wake uweze kuwa  na tija.

Hawa saidi kasimu kutoka jumuiya ya wakulima wa mbogamboga pamoja na ufugaji (uwamwema) amesema lengo la ziara hiyo ni kuwajengea uwezo wafugaji wa kuku  ili waweze kufuga kwa utaalamu wa kisasa hivyo amewataka wafugaji kuchangamikia fursa zinazotolewa na serikali pamoja na taasisi binafsi ili kujiendeleza katika ufugaji wao.