WAISLAM KUENDELEZA AMANI ILIOPO ILI KUIEPUSHA NCHI KUINGIA KATIKA MIFARAKANO

 

Naibu mufti mkuu wa malawi sheikh  shwaibu ibrahim amewataka waislam kuendeleza amani iliopo ili kuiepusha nchi kuingia  katika  mifarakano ya wenyewe kwa wenyewe.Akifunga ijitimai ya kimataifa huko ole kianga pemba  sheikh  shaibu amesema iwapo nchi haitokuwa na amani haiwezi kupiga hatua za maendeleo na hata wageni watashindwa kuingia nchini.

Amesema amefurahishwa na hatua ya jumuiya ya fiysabillah tabligh markaz ya kuendeleza masuala ya ijitimai kwa kila mwaka kwani jambo hilo limekuwa likiwakutanisha waislam kutoka nchi mbali mbali .Mwenyekiti wa jumuiya ya fiysabillah tabligh markaz amir ali khamis na makamu mwenyekiti amir wakati hassan  wakizungumzia changamoto za jumuiya hiyo wamesema wanashangazwa na baadhi ya watu wanaotoa maneno ya kuvunja moyo juu ya kufanywa kwa  ijitimai  kwa kudai kuwa wamekuwa wakitumia fedha  kwa mambo yao binafsi.Aidha uongozi huo umevipongeza vyombo vya habari katika kuhakikisha wananchi wanapata habari katika shughuli nzima ya ijitimai hadi kumalizikaIjitimai ya kimataifa iliofanyika kwa muda wa siku tatu imewashirikisha waumini kutoka uganda, kenya, malawi, mikoa mbali mbali ya tanzania  bara na wenyeji zanzibar