WAISLAM WAMEHIMIZWA KUTEKELEZA MAMBO MEMA YENYE KULETA MANUFAA KWAO NA JAMII

 

Waislam wamehimizwa kutekeleza mambo mema yenye kuleta manufaa kwao na jamii ili kuhakikisha wananufaika duniani na akhera.Nasaha hizo zimetolewa na mkuu wa mkoa wa mjini magharib mh. Ayoub muhamed, wakati wa kikao cha uzinduzi wa uchangishaji wamaandalizi ya ijitimai ya kimataifa inayotarajiwa kufanyika Tarehe 16 mwezi wa tatu mwaka huu ole kianga pemba.

Aidha mh. Ayoub amewataka wazazi kuhakikisha wanawasimamia watoto wao katika malezi ili wawe na mwenendo mzuri katika jamii.Akizungumzia suala la udhalilishaji mkuu wa mkoa amewataka waislam kuwa mstari wa mbele katika kupinga vitendo hivyo kwani vimekuwa vikiathiri jamii na taifa kwa ujumla.Mwenyekiti wa jumuiya ya fiysabillah tabligh markaz amir ali khamis na makamu mwenyekiti wake amir wakati, wamesema lengo la uzinduzi huo ni kuongeza nguvu za pamoja katika ukusanyaji wa michango ili kuhakikisha ijitimai hiyo inafanyika.Katika uzinduzi huo na mkuu wa mkoa huyo ameahidi kuchangia shilingi milioni moja katika ijitimai hiyo.