WAISLAMU KISIWANI PEMBA WAMETAKIWA KUFAHAMU UMUHIMU WA UTAFITI

 

 

Waislamu kisiwani Pemba wametakiwa  kufahamu umuhimu wa utafiti wa mafuta na gesi asilia unaoendelea kisiwani humo  na kutoa  ushirikiano ili  zoezi la utafiti huo liweze kufanikiwa.

akizungumza na waislamu katika msikiti  wa wingwi mjananza  kwenye hafla ya mashindano ya Quran Sheikh Said amesema suala la utafiti limepewa umuhimu katika uislamu hivyo waislamu wasibeze juhudi zozote za utafiti zinazofanywa…

amesema kitabu kitukufu cha Quran kimeelezea umuhimu wa utafiti katika rasilimali za nchi kwani lengo lake ni kuwainua wananchi kiuchumi na maisha yao kwa ujumla.

aidha akizungumza na waumini wa Dini ya Kislamu katika msikiti wa kangagani wilaya ya wete sheikha saidi amewaasa waislamu hao kutohusisha suala la tafiti mbali mbali na mambo ya kisiasa akisema suala hilo ni la kitaaluma zaidi…

utafiti wa mafuta na gesi asilia kwa njia ya mitetemo unaoendelea  hapa zanzibar ambao unasimamiwa na kampuni ya ras al khaimah ya Falme za Kiarabu na ambao umekamilika kisiwani unguja sasa unaendelea pemba ukisimamiwa na  kampuni ya BGP kutoka nchini china na  unakadiriwa kuchukua muda wa miezi sita.