WAISLAMU NCHINI PAMOJA NA VIONGOZI WA DINI WAMEHIMIZWA KUTUMIA MIONGOZO YA DINI

Waislamu nchini pamoja na viongozi wa dini wamehimizwa kutumia miongozo ya dini hiyo kusimamia amani na kupambana na kuvitendo viovu ukiwemo udhalilishaji wa kijinsia.
Naibu kadhi mkuu wa zanzibar shekh hassan othman ngwali amesema viongozi hao wamekuwa na ushawishai mkubwa kwa jamii hivyo watumie nafasi zao kuhakikisha masuala hayo yanamalizika ili kulinda maadili.
Sheikh ngwali ambae alikuwa akifungua semina kwa mashekhe, walimu wa madrasa na viongozi wengine wa dini amewataka watoe taaluma katika mahubiri yao kwenye sehemu mbalimbali ikiwemo nyumba za ibada.
Sheikh thabit nouman jongo akizungumzia umuhimu wa amani katika nchi amesema suala hilo ni muhimu katika kufanikisha masuala yote ya kimaendeleo nchini.
washiriki wa semina hiyo amesema mmongonyoko wa maadili imekuwa sababu kubwa ya kuongezeka vitendo vya udhalilishaji katika jamii na kusisitiza ushirikiano wa wadau mbalimbali ili kumaliza kabisa tatizo hilo.