WAISLAMU WAMETAKIWA KUFAHAMU KUWA HIJJA NI NGUZO YA LAZIMA KWA KILA MWENYE UWEZO

 

Waislamu nchini wametakiwa kufahamu kuwa   hijja ni nguzo ya lazima   kwa kila mwenye uwezo kuitekeleza ibada hiyo.Hayo yameelezwa na mlezi wa taasisi ya  talbiya hajj ,umra  sheikh khamis abdul –hamid wakati akizungumza katika muendelezo wa mafuzo ya ibada ya hijja kwa vitendo yaliyofanyika  kidoti  wilaya ya kaskazini ‘a’ unguja.Nao wananchi waliojitokeza katika mafunzo hayo wakaiomba taasisi hiyo kuendelea kutoa mafunzo hayo kila watakapohitajika.