WAJASILIAMALI WAMESISITIZWA KUWEKA MKAZO NA NIDHAMU KATIKA MATUMIZI YA FEDHA ZA USHIRIKA

 

 

Wajasiliamali wa  ushirika wa mungu hakopeshwi waliopo mwaera mtofaani  wamesisitizwa  kuweka mkazo na nidhamu katika matumizi  ya fedha  za ushirika huo ili waweze kufikia malengo  .

Ushauri huo  umetolewa na waziri wa habari  utamaduni utalii na michezo mh rashid ali juma  baada ya kulikagua jengo la ushirika huo amesema migogoro mingi  inayozuka  katika vikundi inatokana  matumizi mabaya ya fedha  na kutokuwepo uwazi katika matumizi halali kwa wanachama ili fedha  hizo ziweze kuwasaidia na wendine .Mh  rashid amewataka wanaushirika hao  kuzidisha  ushirikiano  katika kuendeleza ushirika  huo  pamoja na kujifunza zaidi elimu ya ujasili amali  ambayo inatoa fursa ya kujiajiriMapema  aki yataja  malengo ya  ushirika huo katibu merre mayco  amesema  ni pamoja na kuwaunganisha wajasiliamali kuwa na  nguvu za pamoja katika suala zima la kijikwamua na umasikini pamoja  na kuwatakaka wafadhili kuwawezesha ili waweze kukamilisha jengo lao ushirika  wa mungu hakopeshi  umeazishwa mwaka 2010  na sasa unawanachama   58