WAJASIRIAMALI KUZALISHA BIDHAA ZENYE KUHITAJIKA KATIKA SOKO

 

 

Waziri  wa  kilimo   maliasili mifugo na  uvuvi mh Hamad  Rashid  Mohammed amewataka wajasiriamali  kuzalisha bidhaa  zenye  kuhitajika katika  soko la biashara pamoja  na jamii inayowazunguuka .

Akizunguuka  katika  ufunguzi wa  mkutano  mkuu wa mtandao wa  wajasiriamali vijijini vicoe amesema ni vyema  kufanya  utafiti juu  ya  bidhaa  wanazotaka  kuzizalisha  kutokana  na fursa  ziliopo  vijijini ili  zipate  soko.la uhakika

Amewataka wajasiriamali kuacha tabia ya  kuzalisha  bidhaa  zinazofanana  kwani zinaondosha ubora wa soko na  kutokidhi viwango

Viongozi  na wanachama wa  mtandao  huo  wamesema  bado  wanahitaji kuongezewa  nguvu  zaidi na serikali ili kuwezesha  kupata nyenzo za  kuviimarisha  vikundi  vya  ujasiri amali vya vijijini

Mtandao wa  wajasiriamali  vijijini  unazaidi ya vikundi  20  vyenye kujishughulisha na  ukulima ,ufugaji  na kazi za  mikono katika  vijiji  vyao kwa  lengo la kujikomboa  kiuchumi.