WAJASIRIAMALI WAMESHAURIWA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA MTANDAO

Vijana wajasiriamali wameshauriwa kutumia teknolojia ya mtandao ili kutangaza na kutanua biashara zao wanazozalisha .
Akitoa mada kuhusu biashara ya mtandao kwa wajasiariamali vijana mwanaharakati wa masula ya vijana seif gharib amesema dunia imebadilika kiteknolojia hivyo mfumo huo ndio wenye fursa nyingi za kukuza kipato.
Mratibu wa mafunzo hayo yaliyoandaliwa na jumuiya ya kupambana na matatizo ya vijana zafyco mustafa sharif amesema wameamua kutoa mafunzo hayo kwa vijana ili kuwatanua mwanga juu ya fursa za kukuza mitaji na kujitangaza.
Baadhi ya vijana walishiriki mafunzo hayo wamesema wamefarijika kupata mafunzo hayo na kuomba kuendelezwa hasa kwa walioko vijijini.