WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI KUTORIDHISHWA NA MUENDELEZO NA USIMAMIZI WA KESI ZA RUSHWA

 

Wajumbe wa baraza la wawakilishi wameelezea kutoridhishwa na muendelezo na usimamizi wa kesi zinazohusiana na vitendo vya rushwa na uhujumu uchumi ambapo kuna jumla ya kesi 187 ambazo hazijatolewa maamuzi.Wakichangia ripoti ya utekelezaji wa majukumu ya mamlaka ya kuzuwia rushwa na uhujumu uchumi (zaeca), iliyowasilishwa na waziri wa nchi ofisi ya rais katiba, sheria, utumishi wa umma na utawala bora, wajumbe hao wamehoji kinachasababisha kuchelewa kusikilizwa kwa kesi hizo na kukosekana taarifa za hukumu zilizotolewa kuhusiana na kesi hizo.Akiwasilisha maoni ya kamati, makamu mwenyekiti wa kamati ya sheria, utawala bora na idara maalum, mh. Mwantatu mbarak khamis, ameishauri zaeca kufuatilia makosa yanayohusiana na  uhujumu wa uchumi yanayofanywa kwa njia ya mitandao.

Ripoti hiyo iliwasilishwa na waziri wa nchi ofisi ya rais katiba sheria utumishi wa umma na utawala bora, mh. Haroun ali suleiman.Wakati huo huo naibu spika wa baraza la wawakilishi mh. Mgeni hassan juma ametangaza majina mapya ya kamati za baraza la wawakilishi, ambapo baadhi ya kamati zitaongozwa na wenyeviti wanawake kwa mara ya kwanza.