WAJUMBE WA KAMATI YA UANGAMIZI WA DAWA ZA KULEVYA WAMETAKIWA KUWA WADILIFU

 

Wajumbe wa kamati ya uangamizi wa dawa za kulevya ya tume ya kitaifa  ya kuratibu na kudhibiti wa dawa za ulevya Zanzibar wametakiwa kufanya kazi  kwa uadilifu kwa kuthamini  maslahi ya nchi na vijana ambao ni wahanga wakubwa wa utumiaji wa dawa hizo.

Akizindua kamati hiyo kwa niaba ya waziri wa nchi ofisi ya makamo wa pili wa Rais mkuu wa mkoa mjini magharibi mhe Ayoub Mohammed Mahmoud hapo katika ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka amesema kamati hiyo ina nafasi kubwa ya kuinusuru jamii yetu kwa kuangamiza dawa za kulevya kwa kufuata utaratibu unaokubalika kwa mujibu wa sheria za nchi yetu na za kimataifa.

Mhe ayoub ameeleza kuwa nchi yetu inkabiliwa na madhara mengi yatokanayo na matumizi ya biashara haramu ya dawa za kulevya na nguvu kazi ya jamii imekuwa ikipotea na kupelekea nchi kutajika vibaya kutokana na janga la dawa za hizo.

Aidha mkuu wa mkoa amewasisistiza kanuni iliyopo imekuja kuondoa matendo machafu yanayofanywa na baadhi ya waliopewa dhamana ya kutunza dawa haramu pindi zinapokmatwa wakati hatua zikiendelea za kisheria.

Mwenyekiti wa kamati ya uangamizi wa dawa za kulevya ya tume ya kitaifa ya uratibu na udhibiti wa dawa za kulevya zanzibar ambae pia nia mkurugenzi wa mashtaka nd ibrahim mzee ibrahim amesema tayari zimeshaandaliwa kanuni ambazo zinatoa utaratibu wa kisheria wa kufanya zoezi la uangamizaji wa dawa za kulevya na limeshatolewa katika gazeti la serikali likiwa tangazo la kisheria nambari 66 la mwaka huu.

Kanuni hiyo imetengenezwa kutekeleza matakwa ya kifungu cha 49 cha sheria namba 9 ya mwaka 2009 ambacho kimeipa uwezo tume kuandaa utaratibu wa kuangamiza dawa za kulevya kutoka kwenye uhifadhi wa kisheria.