WAKAANGAJI WA SAMAKI WAMEIOMBA SERIKALI KUWATAFUTIA MFANYABIASHARA WA KUSAMBAZIA GESI KWA BEI YA KIWANDANI

Wakaangaji wa samaki katika soko la kimataifa la feri jijini dar es salaam wameiomba serikali kuwatafutia mfanyabiashara mmoja ambae atabeba jukumu la kuwasambazia gesi kwa bei ya kiwandani.
Ombi hilo limekuja kufuatia kupanda kwa bei ya nishati hio hali iliyosababisha kukosekana kwa wateja wanaohitaji huduma ya kukaangiwa samaki sokoni hapo.
Zbc ilifika sokoni feri na kuzungumza na mwenyekiti wa wakaanga samaki ali mshirazi mbonde ambae alikuwa na haya ya kusema.
Kwa upande wakemfanyabiara na mjumbe wa sokoni zoni namba 6 mfaume ali namkopa amesema ombi lao la kupunguziwa bei au kutafutiwa msambazaji mmoja wa nishati hio linatokana na kuwa wao si wafanyabiashara bali ni watoa huduma.
Huduma ya ukaangaji wa samaki kwa kutumia majiko ya gesi katika soko la kimataifa la feri ulihama kutoka matumizi ya nishati ya kuni na mkaa kufuatai agizo la serikali la kuwataka kutumia nishati ya gesi lengo likiwa ni kwenda sambamba na utunzaji wa mazingira nchini lakini sasa matumizi ya nishati hio yameonekana kuwa ni changamoto kwa wakaanga samaki hao.