WAKAAZI WA KIJIJI CHA MGONJONI WAMEANZA KUNUFAIKA NA HUDUMA YA MAJI SAFI

wakaazi wa kijiji cha mgonjoni wameanza kunufaika na huduma ya maji safi kufuatia kukamilika ujenzi wa kisima cha kusambaza huduma hiyo.
kisima hicho kimejengwa na mamlaka ya maji zanzibar ikiwa ni agizo la serikali la kuhakikisha kunafikishwa huduma muhimu ikiwemo ya maji katika kijiji hicho chenye kiasi ya wakaazi 250.
wakaazi hao walikuwa wakilazimika kupata huduma hiyo katika mazingira magumu ikiwemo kutumia visima vya asili hali iliyokuwa ikiwakwaza katika maisha yao ya kila siku hasa kwa akina mama na watoto.
naibu waziri wa maji, ardhi na mazingira mh: juma makungu juma amezindua kisima hicho kilichongharimu shilingi milioni 25 ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya maji na kusisitiza utunzwaji wa miundombinu huku akiwaomba wadau mbalimbali kusaidia maendeleo ya kijiji hicho na zanzibar kwa ujumla
mkuu wa wilaya ya kaskazini issa juma ali na mwakilishi wa jimbo la kiwengwa bibi asha abdalla mussa wameomba wakaazi wamgonjoni kuendelea kuwa wastahamilivu kwa baadhi ya changamoto kwa kuwa serikali inaendelea kuzitatuwa ikiwemo ujenzi wa kituo cha afya.