WAKAAZI WA KISIWA PANZA WAMEIOMBA SERIKALI KUANGALIA UPATIKANAJI WA HUDUMA MUHIMU

Wakaazi wa kisiwa panza wameiomba serikali kuangalia kwa ukaribu upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii katika kisiwa hicho ikiwemo tatizo la usafiri.
Wakizungumza na zbc ilipofanya ziara katika kijiji hicho wamesema wamekuwa wakikabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo kutokuwa na usafiri wa uhakika ambapo kwa sasa wanatumia vidau vidogo kuvuka katika ameneo mengine ambavyo vimekuwa si salama kwa maisha yao.
Aidha wamesema tatizo la kuingia kwa maji chumvi katika kisiwa hicho linakwamisha shughuli zao za kilimo na kusababisha kushindwa kuzalisha kwa wingi hali inayowapa ugumu wa kipato.
Wamesema kutokana na hali hiyo wengi wao wamejiingiza katika shuguli za uvuvi hivyo wameziomba mamlama husika kuangalia namna ya kukabiliana na hali hiyo.