WAKAAZI WA MGOGONI WETE KUSHIRIKIANA KUONDOA HITILAFU WALIZO NAZO

 

Mkuu wa Wilaya ya Wete nd. Abeid Juma Ali amewataka wakaazi wa shehia ya mgogoni wilaya ya wete kushirikiana na kuondoa hitilafu walizo nazo panapotokezea mgogoro kati yao.

Akizungumza na wakaazi hao juu ya mgogoro wa msikiti uliozuiwa na serikali usiendelee kujengwa amesema lengo la serikali ni kuangalia maslahi ya wananchi kwa kuwapa makazi bora na huduma muhimu za kijamii.

Wakaazi wa shehia hiyo wameiomba serikali kuliangalia kwa kina suala hilo ili lisilete usumbufu miongoni mwa wakaazi hao.

Kaimu mkurugenzi baraza la mji wete bibi salma abuu amewataka wananchi kuwa wastahamilivu kwani serikali  inalifanyia kazi suala hilo na itakapokamilika itatoa taarifa kamili.