WAKAAZI WA NYUMBA ZA KIWANDA CHA SUKARI MAHONDA WATEKELEZE AGIZO LA SERIKALI

 

Kaimu mkuu wa wilaya ya kaskazini b hassan ali kombo amewataka wakaazi wa nyumba za kiwanda cha sukari mahonda watekeleze agizo la serikalim la kutola katika nyumba hizo.

Nyumba hizo ziizojengwa na serikali mwanzoni mwa kujengwa kiwanda hicho zipo katika maeneo mahonda,kitope na mwanakombo mkoa kaskazini unguja.

Kaimu mkuu wa wilaya ametoa agizo  wakati akizungumza na wakaazi wa nyumba hizo na kusema hawastahili kuishi katika nyumba kwa vile muda wa kuishi humo sasa umemalizika.

Amesema watu wanaostahilikuishi katika nyumba hizo ni wafanyakazi wa kiwanda cha sukari tu nasivyenginevo na ametaka ifikapo siku ya jumane wakazi wote hao iwe wameshatoka na kila kilicho chao na   funguo wakazikabidhi katika  afisi ya mkuu wa wilaya kaskazini ‘b’.

Hata hivyo wakaazi wa nyumba hizo wameiomba serekali ya wilaya kuwapa muda kidogo ili kufanya  matayarisho ya kuhama