WAKAAZI WA SHEHIA YA CHUINI NA MAENEO JIRANI WAMEANZA KUNUFAIKA NA HUDUMA YA MAJI

 

Wakaazi   wa  shehia ya  chuini na maeneo jirani wameanza  kunufaika  na  huduma  ya  maji kufuatia  kukamilika  kwa  kazi ya kuchimba visima na vifaa  vya  kusambazia maji  ndani ya shehia hizo.

Wakaazi wa maeneo hayo wamesema kukamilika kwa kazi hizo kutawaondoshea usumbufu wanaoupata kwa muda mrefu na wameshukuru viongozi wa jimbo hilo kwa kukamilisha mradi huo.

Mbunge wa jimbo la Mfenesini Mh Kanal Mstaafu Masoud  khamis amewasisitiza  wananchi wa shehia hizo kuwa walinzi wa mradi huo ili miundombinu hiyo isije ikaharibiwa na wahalifu.

Jumla ya visima tisa vimechimbwa katika jimbo la mfenesini vikiwa na thamani ya shilingi milioni 63 ikiwa ni katika utekelezaji wa ahadi za viongozi wa jimbo hilo ya kuwapatia huduma bora na kuwaondoshea usumbufu wananchi.